Header

Baada ya Ushindi wa Tuzo ya BET, Rayvanny na Jason Derulo waingia Studio.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB Rayvanny, ni wiki kadhaa tangu kukutana kwake na Staa wa ngoma ya ‘Swalla’ kutoka Marekani Jason Derulo katika msimu mpya wa awamu ya tano wa Coke Studio nchini Kenya na sasa wamekutana tena Studio kukutanisha sauti zao katika kazi ya pamoja.

Jason Derulo na Rayvanny wakiwa Coke sStudio nchini Kenya

Kwa mujibu wa picha, imeonekana tayari wawili hao wameimgia studio kufanya kazi ambapo katika kuhakikisha hiko linakamilika meneja wa shughuli za kimuziki wa lebo hiyo Hamis Tale Tale a.k.a Babu Tale ameonekana kuwa sambamba katika hilo.

Hata hivyo Rayvanny kwa mfululizo huo wa matukio makubwa huko Marekani ni dalili tosha kuwa kiwango cha muziki wake kinazidi kupanda kwakuwa hii ni mara baada ya kutia kibindoni tuzo yake ya ‘Best International Viewers Choice Award’ BET Awards 2017.

Comments

comments

You may also like ...