Header

Enock Bella ahaha baada ya ngoma yake kuvuja

Kwa mujibu wa Enock Bella, wimbo wake Mkuyu umevuja. Msanii huyo wa Yamoto Band ameiambia Dizzim Online kuwa wimbo huo umetoka bila idhini yake.

“Unajua mwenyewe nilikuwa sijui kabisa kama ngoma imetoka na sijui nani alikuwa ameevujisha,” amesema. “Kuna mshikaji wangu mmoja wa Kenya alinipigia na kuisifia ngoma yangu, ki ukweli nilishaanga sana kwasababu nilikuwa bado sijaachia na yeye aliipata kupitia magroup ikanibidi nimtafute Maxmizer nikamuuliza juu ya ngoma yangu kuvuja lakini hakusema hasa ni nani na alijionesha kama hajui kitu chochote,” ameongeza.

“Kiukweli tulikolomeana sana, ila ndio basi imeshatokea.”

Pamoja na yaliyotokea, Bella amewaomba mashabiki waendelee kuisupport ngoma hiyo.

Comments

comments

You may also like ...