Header

Jux hana mpango wa kuanzisha label yake muda huu

Baada ya kuhitimu shahada yake ya kwanza wiki hii nchini China, Jux aliahidi kuwekeza zaidi kwenye biashara na muziki wake. Hata hivyo, katika mipango hiyo, kuanzisha label na kusaidia wasanii wachanga, si kitu anachofikiria.

Ameimbia Dizzim Online kuwa anachokifanya sasa ni kuijenga kwanza brand yake kabla ya kufikiria kusaidia wasanii wengine. “Ni kweli kwa msanii ambaye umepiga hatua fulani kwenye muziki kama mimi ni vizuri kusaidia wasanii wenzako, lakini kwa mimi sasa hivi bado,”amesema. “Nataka nijiweke vizuri zaidi. Watu wanaweza kufikiria labda nipo tayari kufanya hivyo, ndio naweza kuwa nipo tayari lakini sio utayari ambao nautaka mimi. Sitaki mtu akifika kwenye mikono yangu namsimamia awe anayumba kwa chochote, yaani kila kinachohitajika kwenye kazi yake basi kiwe kinafanyika kwa wakati muafaka,” ameongeza.

“So bado naendelea kujipanga, nitakapokuwa tayari nitatangaza na msanii ambaye atakuwa na kipaji ambacho mimi nakiona na watu wote basi tutasaidia,” amesisitiza muimbaji huyo wa Umenikamata.

Comments

comments

You may also like ...