Header

Remy Ma amnyoosha Nicki Minaj kwenye Tuzo za BET 2017

Rapa wa kike na mkali wa michano katika ngoma kama ‘Money Showers’ na ‘All The Way Up’ anayetajwa kuwa katika bifu zito na mchanaji mwenzaje Nicki Minaj, Remy Ma ameshinda tuzo kubwa na kuwaacha mikono mitupu wenzake katika kipengele cha ‘Best Female Hip Hop Artist’ kwenye tuzo za BET 2017.

Remy Ma alipokuwa akitoa Neno(BET Awards 2017)

Tuzo hizo zilizofanyika Jumapili ya tarehe 25 mwezi Juni mjini Los Ageles , kupitia kipengele hicho joto lilikuwa juu kwa mashabiki wa Remy Ma na Nicki Minaj kwakuwa walingoja kwa hamu jibu la kujua nani atamchakaza mwenzake ambapo katika kutaja ushindi wa kipengele hicho kwa mujibu wa kura za mashabiki BET hawakusita kumtunuku tuzo Remy Ma.

Remy akitoa neno la shukrani kwa watu wake wa karibu ambao ni mumewe Papoose na rafiki wake mkubwa Fat Joe na wengine hakuacha kumtupia kijembe Nick. Wakali wengine waliokuwa katika kipengele hicho alichoshinda Remy mbali na Nicki ni pamoja na Cardi B, Young M.A, Missy Elliott.

Hata hivyo Remy tangu kutoka kwake jela hii ni tuzo yake kubwa katika ukali wake wa kufanya muziki na kuonekana kumyumbisha Nicki Minaj tangu alivyorudi rasmi kwenye game la muziki wa Marekani na kua dalili za kuendelea kufanya vizuri.

Comments

comments

You may also like ...