Header

Stephen Curry aendeleza Ubabe kwa LeBron James nje ya Uwanja

Stephen Curry amempiku mpinzani wake LeBron James katika Tuzo za BET zilizotolewa Juni 25 mwaka huu nchini Marekani kwenye kipengere cha mwanamichezo bora wa kiume wa mwaka 2017.

Stephen Curry na LeBron James katika NBA Final

 

Curry, 28 ameshinda tuzo hiyo mbele ya wanamichezo wenzake ambao ni Cam Newton wa Carolina Panthers, Odell Beckam Jr wa New York Giants , Russel Westbrook pamoja na mpinzani wake LeBron James wa Cleveland Cavaries.

Nyota huyo wa Golden State Warriors amekua na msimu mzuri na timu yake akiisaidia kushindwa ubingwa Fainali za Ligi kuu ya kikapu nchini Marekani dhidi ya Cavs mapema mwezi Juni mwaka huu. ikiwa ni tuzo yake mara tatu mfululizo 2015, 2016 na 2017

Mcheza Tenisi Serena Williams ameshinda tuzo ya Mwanamichezo bora wa mwaka kwa upande wa Wanawake akiwapiku wapinzani wake Gabby Douglas, Simone Biles, Skylar Diggins pamoja na dada yake Venus Williams.

Serena Williams akishangilia ubingwa wa Australian Open 2017

 

Comments

comments

You may also like ...