Header

Vera Sidika atikisa mitaa ya Hollywood Marekani

Mrembo mwanamitindo na mfanya biashara maarufu  kutoka nchini Kenya, Vera Sidika ametingisha mtandao hasa kwa wafuasi wake mara baada ya kupost picha akiwa katika pozi la kujipamba kwa nyoka mkubwa mjini L.A, California nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa kapendeza katikati ya mtaa maarufu wa Hollywood(Hollywood Boulevard) Vera alipost picha akionekana amepozi katikati ya umati wa watu waliokuwa busy na shughuli zao huku baadhi wakijiuliza maswali kadhaa kuhusu mrembo huyo kwa jinsi alivyo jiachia na nyoka shingoni huku akipigwa picha bila kujali nani amuangalia.

Hata hivyo kikubwa mbali na uwepo wake katika mtaa huo na pambo lake la nyoka picha hiyo ya Vera ilipamba moto kwakupata maoni mengi kuhusu mtoto aliyeonekana akiwa katika kikapu cha kushukuma akisumkumwa na mwanaume huku alionekana akiwa ni mwenye kumkodolea macho kuelekea upande wa nyuma wa Vera kwa mujibu wa picha.

Comments

comments

You may also like ...