Header

Binti wa Sylvester Stallone ‘Rambo’ aongeza mwaka mmoja wa utu uzima

LOS ANGELES, CA - FEBRUARY 10: (L-R) Model Sistine Stallone, actor Sylvester Stallone and Sophia Stallone attend Saint Laurent at the Palladium on February 10, 2016 in Los Angeles, California for the Saint Laurent Los Angeles show. (Photo by Larry Busacca/Getty Images for SAINT LAURENT)

Sistine Rose Stallone ni mrembo, mwanamitindo na mtoto wa staa kutoka Marekani anayetajwa kwa ukongwe wa filamu za Hollywood Sylvester Stallone ambaye wengi wanamfahamu zaidi kwa jina la ‘Rambo’.

Sistine mwaka jana tarehe 27 Juni aliingia rasmi kwenye orodha ya wanaotambulika kuwa mtu mzima kwakuwa alitimiza umri wa miaka 18 ambapo tarehe ya leo kwa mara nyingine anasherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwake.

Sistine Stallone ni zao la wanandoa Sylvester Stallone na Jennifer Flavin waliobahatika kupata watoto watano, na idadi ya waliobaki ni wanne ambao ni Sophia Rose Stallone, Seargeoh Stallone, Scarlet Rose Stallone huku kijana mkubwa wa kiume Sage Stallone aliyefuata nyayo za baba yake za uigizaji alifariki mwaka 2012 akiwa ni mwenye umri wa miaka 36.

Comments

comments

You may also like ...