Header

Chris Brown na Karruache Tran wakaa mbali mbali kwenye BET Awards

Chris Brown na ex wake, Karruache Tran hawakuonana wala kukutana Jumapili kwenye tuzo za BET licha ya wote kuwepo. Kituo hicho cha runinga, kilitengeneza mazingira kuwasaidia wawili hao wasikutane kutokana na hukumu iliyotolewa hivi karibuni ambapo Chris hatakiwi kumsogelea Karruache kwa miaka mitano.

Kwa mujibu wa TMZ, moja ya mpango huo ni kumweka Karrueche kwenye chumba maalum wakati Brown akitumbuiza nyimbo zake “Privacy” na “Party” akiwa na Gucci Mane. Pia mrembo huyo anadaiwa kutoiangalia show ya ex wake.

Brown anatakiwa asimsogelee Tran kwa umbali wa yards 100 na muda wote wakati wa show alikuwa backstage. Tran alipanda kutoa tuzo. Hata hivyo baada ya show kambi ya Brown ilikwaruzana na ile ya msanii wa kundi la Migos, Quavo anayedaiwa kuwa na uhusiano na Tran.

Comments

comments

You may also like ...