Header

COSAFA yaondoa kiingilio, kuwaona Stars ni bure

Kamati ya maandalizi ya Michuano ya COSAFA inayoendelea nchini Afrika Kusini imetangaza kuwa Michezo yote iliyosalia ya raundi ya kwanza kuazia itakayofanyika Jumanne Juni 27 haitakuwa na kiingilio, mashabiki watapatiwa tiketi za bure kutazama mechi hizo.

Raundi ya kwanza inatarajiwa kumalizika Juni 30 wakati timu moja kutoka kila kundi ndiyo itakayofuzu kutinga hatua ya robo fainali ikiungana na timu za Zambia, Afrika ya Kusini, Botswana, Namibia, Lesotho pamoja na Swaziland.

Mechi ambazo za raundi ya kwanza ambazo ni bure kuzitazama ni pamoja na;

27/6   Malawi vs Mauritius
27/6   Angola vs Tanzania
28/6   Zimbabwe vs Madagascar
28/6   Seychelles vs Mozambique
29/6   Tanzania vs Mauritius
29/6   Malawi vs Angola
30/6   Mozambique vs Madagascar
30/6   Zimbabwe vs Seychelles

Katika Mashindano hayo Timu ya Taifa ya Tanzania inashiriki kama timu mwalikwa, itashuka uwanjani hii leo kucheza dhidi ya Angola katika kundi A majira ya saa mbili na nusu za usiku. Mchezo mwingine katika kundi hilo utakua ni kati ya Angola dhidi ya Mauritius.

 

Comments

comments

You may also like ...