Header

Idris Sultan awakumbusha Navy Kenzo, Diamond na wengine kufunga ndoa

Idris Sultan amewakumbusha Diamond Platumz, Nahreel na wengine waliopo kwenye uhusiano wa muda mrefu na wapenzi wao kufunga ndoa. Akiongea na Dizzim Online, mtangazaji na mchekeshaji huyo amedai kuwa maisha wanayoishi hayana tofauti na kufanya uzinzi.

“Unajua wasanii wengi ni wazinzi, wengi wao hawajaoa wala kuolewa wanapigapiga tu, so nawakumbusha,” amesema mshindi huyo wa shindano la Big Brother Africa mwaka 2014.

“Lakini pia nawaombea kwa mwenyezi Mungu kidogo waweze kuhalalisha mahusiano yao, yaani waoe au kuolewa na mzizi mkuu kabisa ni Diamond hajaoa na ana watoto wawili na wengine wengi akina Navy Kenzo, labda hao wameoa halafu hawajatuambia, lakini si tunajua kwamba bado wazinzi. So mimi nawashauri angalau tuhalalishe mahusiano yetu, yaani hivi tulivyomaliza mwezi vizuri basi tuendelee hivi hivi, tuendelee kufanya kufanya ambo mazuri,” amesisitiza.

Aidha ameongeza,” Najua mi pia ni mzinzi kama wazinzi wengine tu na najitahidi kwenye suala la uzinzi ili kuilinda dini yangu. Najua tunajisahau sana hasa tunapokuwa maarufu lakini mi najitahidi sana kama ambavyo mnajua mi ni mtoto wa Imam, nimekulia kwenye dini, so vitu vingi navifahamu.”

Comments

comments

You may also like ...