Header

TID aipa baraka ngoma ya Quick Rocka, ‘Watasema’

Hatimaye TID ameipa baraka ngoma mpya ya Quick Rocka aliyowashirikisha OMG, Watasema. Ngoma hiyo imechukua kionjo cha wimbo wa zamani staa huyo, Watasema Sana aliomshirikisha Nazizi. Awali, kupitia Instagram, TID alimchimba mkwara Quick kuwa anataka fidia ya shilingi milioni 20 kwa kutumia wimbo wake bila ruhusa.

“Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema. Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo,” aliandika.

Jumanne hii, TID na Quick Rocka walialikwa kwenye kipindi cha XXL kupitia Clouds FM kuzungumzia suala hilo. Mnyama amedai kuwa ni kweli alikuwa amepanic baada ya kuona wimbo wake umetumika kwakuwa ulimgharimu takriban shilingi milioni 1 na nusu kuutayarisha katika studio za Home Boyz. Amedai kuwa baada ya Quick kumtafuta kwa mazungumzo, aliamua kuufungua moyo wake kwasababu ya kupenda muziki mzuri.

Naye Quick amesema baada ya kuumaliza wimbo huo alimpigia simu TID kumwambia kuna kitu amekifanya lakini hakumweleza zaidi. Amemsifia nguli huyo wa Bongo Flava kwa busara zake na kuipa baraka ngoma yake, Watasema.

“Tushapata Blessings from our brother @tidmusic….Haya mliokuwa mnasema endeleeni ila mwisho mtalala,” ameandika Quick kwenye Instagram.

Comments

comments

You may also like ...