Header

AKA ampa Bata mpenzi wake Bonang kwenye Hotel ya Trump

Ukizungumzia moja ya couple maarufu na yenye nguvu nchini Afrika Kusini katika kiwanda chao cha Burudani hautaacha kumzunguzia rapa AKA na mpenzi wake ambaye ni mtangazaji Bonang Matheba.

Inakumbukwa kuwa Dizzim Online kupitia ukurasa wake wa Twitter ilikupa taarifa kuwa rapa AKA ana mpango wa kumpa bata la hatari mpenzi wake Bonang mjini New York katika kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake kwakuwa tulipata taafifa hizo kupitia akaunti ya AKA mwenyewe.

 

Basi, ilipofika tarehe hiyo ya Bonang kutimiza umri wa miaka 30 AKA akatimiza ahaadi yake ambapo kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa Afrika Kusini wa TshisaLIVE imekadirikwa kuwa wakiwa mjini New York wametumia pesa isiyopungua 6000 USD kwa malipo ya usafiri wa ndege na Malazi katika Hotel maarufu ya ‘Trump International Hotel & Tower New York’ kisha kupata mlo wa nguvu kwenye mgahawa maarufu wa Nello.

Hata hivyo kwa matumizi hayo kama zawadi kwenda kwa mpenzi wake Bonang, AKA ameonekana ni wazi ana mapenzi ya dhati na ampa thamani kubwa mpenzi wake huyo.

Comments

comments

You may also like ...