Header

Pogba ndani ya Video ya Desiigner (+Video)

Kampuni ya Adidas imemtumia Mchezaji Paul Pogba wa Manchester United pamoja na Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Sidney Royel Selby III maarufu kama Desiigner katika kuipa nguvu na kuitangaza Jezi mpya ya Manchester United itakayotumika msimu wa 2017/2018.

Pogba akiwa amevaa Jezi mpya ya Manchester United itakayotumika msimu Ujao 2017/2018

 

Wakali hao wawili wameonekana pamoja kwenye wimbo mpya wa Desiigner unaofahamika kwa jina la ‘Outlet’ ambao Mandhari ya nyimbo hiyo kwa asilimia kubwa imefanyika katika uwanja wa Old Traford ambao ni uwanja wa nyumbani wa Manchester United huku Pogba akitumika kama mshiriki mkuu katika video hiyo ambayo Jezi ya Manchester United ya Msimu ujao imeonekana kwa asilimia kubwa ikiwa imevaliwa na Desiigner pamoja na Pogba.

Pogba, 24 ni moja kati ya mabalozi wa kampuni ya Adidas, dili alilolipata alipojiunga na Manchester United Mwanzoni mwa msimu uliopita akiweka rekodi ya kuwa Mchezaji ghali Duniani.

Wachezaji wa Manchester United wakiwa wamevaa jezi mpya

 

Comments

comments

You may also like ...