Header

Witnesz: Mimi na Ochu tumeivana zaidi ya kawaida

Rapper wa kundi la zamani la Wakilisha, Witnesz aka Kibonge Mwepesi, amezungumzia vitu anavyojivunia pindi anapofanya kazi na mpenzi wake Ochu ambaye ni muimbaji pia. Ameimbia Dizzim Online kuwa Ochu ni mwanaume anayemwelewa zaidi.

“Unajua unapokuwa na mpenzi wako na mnafanya kitu cha aina moja unakuwa unaelewa zaidi na yeye inakuwa rahisi kukuelewa wewe tofauti na watu wa nje wanavyokuchukulia,” amesema. “Pia inakuwa rahisi yeye kujua mipaka yake katika jamii na kwangu pia. So nafurahia sana kufanya kazi na Ochu na ananipa support kubwa kuliko mtu yoyote. Na kitu kingine ambacho watu hawakijui sisi mpaka password za kila sehemu kila mtu anaijua ya mwenzake. Mimi najua password yake na yeye anazijua password zangu za kila sehemu,” ameongeza rapper huyo.

Wetnesz na Ochu wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu huku wote wakifanya biashara na muziki.

Comments

comments

You may also like ...