Header

Baada ya kupata mtoto Linex aahidi kuwa kama Dj Khaled kwa Asahd

Linex ni baba mpya mjini. Wiki hii muimbaji huyo amejaaliwa kupata mtoto wa kiume aliyempa jina Jaheim. Ameiambia Dizzim Online vitu atakavyovifanya kwaajili ya mtoto wake.

“Ukiwa baba kuna vitu inabidi uvibadilishe kwenye maisha yako,” amesema. “Mimi nilikuwa nashangaa mtu akipata mtoto anaanza kubadilika, ila kwa sasa hivi nimejua kwanini. Na mimi kati ya vitu ambavyo nitabadilika ni kama kurudi home usiku mkubwa, sasa hivi nitaanza kurudi home mapema. Zile bata nitaacha kabisa labda niwe na show na kama show basi mwanangu nitamtengenezea mazingira ajue baba yake naenda kazini, pia pesa yangu naipata vipi ili hata nitakaporudi saa tisa usiku au saa kumi ajue nilienda kutafuta pesa,” amesisitiza.

Linex ameongeza, “Mwanangu nimemfungulia account bank, tena kabla hajazaliwa na nataka akishafikisha mwaka mmoja awe tayari kuna vitu anavyofanya vinavyomuingizia pesa. Yeye kama yeye inabidi aingize chapaa, kama baba tu.”

Linex ameahidi July 11 atatoa kitu kama zawadi kwa mwanae.

Comments

comments

You may also like ...