Header

Charlamagne Tha God wa 39 leo, aliwahi kurushiana maneno na Birdman redioni

Mtangazaji maarufu nchini Marekani anayefahamika zaidi kupitia kipindi cha ‘The Breakfast Club’ cha kituo kikubwa cha redio cha mjini New York WWPR-FM au Power 105.1, Charlamagne Tha God ametimiza umri wa miaka 37 ambapo ipo stori kubwa iliyomhusu mwaka jana na kuonekana kuwa katika bifu zito na rapa mfanyabishara Birdman.

Tarehe 22/04/2016 Birdman alikuwa ni mgeni kwenye kipindi cha ‘The Breakfast Club’ na kabla ya kuanza mohojiano na kipindi hicho aliwaonya watangazaji wa kipindi Charlamagne Tha God, Angela Yee, na DJ Envy wakome kulizungumzia vibaya jina lake na kuwataka waliheshimu kila wanapolitaja. Baada ya hilo Birdman aliendelea kurushiana maneno na Charlamagne amara tu alipoulizwa kama wako vizuri katika kuelewana na rapa Rick Ross na Trick Daddy ambao waliwahi kumsema vibaya kupitia kipindi hicho hata Birdman kumtishia Charlamagne. Dakika chache za mwanzoni za mahojiano Birdman alionekana kukasirika zaidi ambapo aligoma kuongea kila alipokuwa akiulizwa swali na Charlamagne na mwisho alishindwa kuvumialia akawataka wapambe wake waondoke bila kufanya mahojiano.

Hata hivyo tukio hilo la Birdman lililoonekana kuwa amekwaruzana zaidi na Charlamagne lilimfanya ajute na kuomba msamaha kisha kuwataka wampange kwenye ratiba ya kurudi kwa lengo la kufanya mahojiano tena ambapo ombi hilo lilikataliwa kwa mujibu wa Dj Envy.

HAPPY BIRTHDAY ‘Charlamagne Tha God’

Comments

comments

You may also like ...