Header

Davido na R.Kelly katika ‘IF’ Remix

Staa wa muziki kutoka Nigeria amezungumziwa tena hasa kwa wapenzi wa muziki wake na muziki wa Afrika kwa ujumla waliokutana na version mpya ya wimbo ambao unatajwa kama Remix Cover ya wimbo wa ‘If’ ambayo katika sauti imesikika kuwa imemshirikisha mkongwe wa muziki wa RnB kutoka Marekani R.Kelly.

Davido anayefanya vizuri na wimbo wake wa ‘Fall’ alishaonekana kutambuliwa na R.Kelly kupitia wimbo wa ‘If’ ambapo ukurasa wa Instagram wa R.Kelly ulitumika akiwa katika location ya Nigeria na kusema kuwa imetumia muda wake kufanya kitu kwenye wimbo huo wa ‘If’ ambacho ni Remix iliyoingia mtandaoni mapema jana.

Hii ni post ya R. Kelly kuhusu kutaka kushiriki katika kuofanya kitu kwenye wimbo wa If wa Davido.

Hata hivyo Davido anaendelea na ziara yake ya Dunia ‘The 30 BILLION WORLD TOUR’ ambapo baada ya show yake ya Djibouti anajipanga kutumbuiza tena tarehe 30 mjini Stockholm nchini Uswidi(Sweeden.)

Comments

comments

You may also like ...