Header

G-Nako adai watu walioshuhudia shooting ya ‘Lucky Me’ waligwaya kumuona akiwa kwenye jeneza

G-Nako amesema hakuogopa kuingia kwenye jeneza wakati wa kufanya video ya wimbo wake Lucky Me. Hata hivyo ameiambia Dizzim Online kuwa baadhi ya watu waliokuwepo karibu waligwaya.

“Watu wajue wakati nafanya vile sikuwa naogopa chochote,” ameimbia Dizzim Online. “Isipokuwa watu tuliokuwa nao location baadhi yao ndo walikuwa wanaogopa na mimi na director tulichokuwa tunakifanya pale ni kuhakikisha ujumbe wetu unawafikia kwa watu kama vile sisi tunavyotaka na tulifanikiwa hilo.”

Kuhusu idea ilipotoka, rapper huyo wa kundi la Weusi amesema, “Mara ya kwanza kabisa idea ilitoka kwa Hanscana, yeye alisema kuwepo na jeneza katika ile video. Sasa ilipokuja jeneza litafanya nini kwenye ile video ndio mimi nikaja na idea ya kwamba niingie kwenye jeneza, ingawa kuna baadhi ya watu waliongea vitu vingi ikiwemo kama kujichulia wakati hawajui kama jeneza ni mbao tu kama zilivyo mbao zingine.”

Comments

comments

You may also like ...