Header

Kanye West apania kurudi kwa kishindo mwaka 2018

Kanye West bado yupo kwenye mapumziko marefu na mwaka huu wote tusitarajie mengi kutoka kwake. Kwa mujibu wa TMZ, Yeezy ataanza kutema cheche zake kuanzia mapema mwaka 2018.

Vyanzo vilivyo karibu naye vimedai kuwa mwakani ataanza ziara yake na tayari yupo kwenye mazungumzo na kampuni ya Live Nation, ile ile iliyosimamia ziara yake ya Saint Pablo mwaka jana, ambayo aliikatisha kutokana na matatizo ya kiafya.

Vimesema kwa sasa Kanye ni mzima wa afya, kiakili na kimwili, zaidi ya alivyokuwa miaka mingi.

Wanasema yuko vizuri sana na ameshapona kutoka kwenye masuala yaliyomfanya aende hospitali mwaka jana. Kwa mujibu wa TMZ, Kanye alienda kupiga kambi Wyoming miezi kadhaa iliyopita kuandaa album yake mpya.

Comments

comments

You may also like ...