Header

Kauli ya Ronaldo yathibitisha ujio wa watoto wake mapacha

Baada ya timu ya Taifa kuondolewa katika Mashindano ya Kombe la Mabara dhidi ya Chile hapo jana, Nyota Cristiano Ronaldo ametangaza kuondoka Mapema nchini Urusi ili kuenda kuungana na watoto wake kwa mara ya kwanza, taarifa aliyoitoa punde tu baada ya Mchezo.

Ronaldo akiwa na timu yake ya Taifa Jana dhidi ya Chile

Ronaldo,32 alitoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook akieleza kuwa baada ya kumalizana na majukumu ya timu ya Taifa sasa anaenda kuungana na watoto wake kwa mara ya kwanza ambao hawajatajwa.

“Nilikua kwenye majukumu ya timu ya Taifa, kama inavokuwaga mwili na akili vinatumika ingawa nilikua nafahamu kuwa watoto wangu wawili wa kiume wamezaliwa”. Nina Furaha sana hatimaye naelekea kuonana na watoto wangu kwa mara ya kwanza. Alisema Ronaldo.

Ronaldo akiwa na Mtoto wake Cristiano Jr pamoja na Mchumba wake Georgina

Taarifa kutoka nchini Marekani zinaripoti kuwa Ronaldo amepata mapacha wawili wa kiume na Mwanamke ambaye hajafahamika(Surrogant Mother) kama ilivyokua kwa mtoto wake wa kwanza Cristiano Jr.

Ronaldo yupo katika mahusiano na Mwanamitindo Georgina Rodriguez ambaye inaripotiwa kuwa Mjauzito kufuatia picha aliyoiweka kwenye mtandao wa kijamii ikionyesha Ronaldo akiwa ameshikilia tumbo la mwanadada huyo.

 

Comments

comments

You may also like ...