Header

Fid Q asema Cheusi Dawa si label ya hip hop tu

Fareed Kubanda aka Fid Q amesema label yake, Cheusi Dawa Entertainment haisaini wasanii wa hip hop peke yake. Ameiambia Dizzim Online kuwa CDE inafungua milango kwa msanii wa aina yoyote.

“Cheusi Dawa mtu yeyote akisikia anajua ni lebo ambayo inakuwa inadeal na wasanii wa hip hop tu, lakini hii si kweli,” amesema. “Cheusi Dawa sasa hivi imefungua milango kwa wasanii wa aina mbali mbali wa sanaa ya muziki, Na huwa mara nyingi tunaepuka kusema tunachagua msanii gani au tutafanya kazi na nani. Mara nyingi huwa tunakuja naye kwenye kazi halafu tunamtambulisha kwa mashabiki kabisa. So watu wawe na subira ndani ya wiki hizi mbili kuna kitu tutafanya,” amesisitiza.

Fid ameongeza, “Lebo yangu haiangalii kipaji peke yake, tunaangalia vitu vingi, nidhamu na vision yake maana msanii anaweza kuwa na talent lakini hana vision wala nidhamu. So hata msanii wa nje ya nchi kama ana vitu hivyo tunaweza kumchukua.”

Hadi sasa Cheusi Dawa imeshamtangaza msanii mmoja, Big Jahman ambaye aliachia wimbo wake Mabundi akiwashirikisha Fid na SaRaha.

Comments

comments

You may also like ...