Header

Jay-Z akiri kuchepuka kwa Beyoncé kupitia Album ya ‘4:44’

NEW YORK, NY - FEBRUARY 20: Beyonce (L) and Jay-Z attend the New Jersey Nets vs New York Knicks game at Madison Square Garden on February 20, 2012 in New York City. (Photo by James Devaney/FilmMagic)

Rapa mkongwe, Baba wa mtoto wa kike Blue Ivy Carter na mapacha mmoja kike na wa kiume ‘Shawn Corey Carter a.k.a Jay-Z leo ameufurahisha ulimwengu wa wapenzi wa muziki wa rap/hip hop kwa kuachia studio album yake ya 13 inayokwenda kwa jina 4:44.

Album hiyo yenye ngoma 10 chini ya utayarishaji wa producer mkongwe ‘No I.D’ iko na wimbo wa kwanza katika orodha unaokwenda kwa jina la ‘Kill Jay-Z’ unatajwa kuwa ni wimbo wenye mistari mistari inayomlenga rapa Kanye West.

Katika album hiyo ya 4:44, idadi kubwa ya mashabiki wamegundua kuwa kipindi ambacho Beyoncé aliachia wimbo wake wa ‘Lemonade’ mwaka Jana ambao alikuwa akimtaja Jay-Z kuwa mwanaume hasiye muaminifu kwake basi Jay-Z katika album hii ametumia wimbo wa tano katika orodha ya nyimbo unaokwenda kwa jina 4:44 kumuomba msamaha Bayonce kwa mapungufu yake katika mahusiano yao na kukubali kuwa alishawahi kuwa mdanganyifu kwenye mahusiano yao.

Jay-Z anasikika kwenye ubeti wa kwanza akichana “Look, I apologize, often womanize

Took for my child to be born

See through a woman’s eyes

Took for these natural twins to believe in miracles…You make it home

We talked for hours when you were on tour/

“Please pick up the phone, pick up the phone”

Said: “Don’t embarrass me,” instead of “Be mine”

That was my proposal for us to go steady

That was your 21st birthday, you mature faster than me

I wasn’t ready, so I apologize”

Hata hivyo album inayopatikana kwenye mtandao unaomilikiwa na Jay-Z mwenyewe wa Tidal imesemekana kuwa wiki kuanzia sasa pia itapatikana kupitia iTune ambapo na utakutana na ngoma kama vile ‘Bam’, ‘4:44’ iliyobeba jina la album, ‘Marcy Me’, ‘Smile’, ‘Legacy’ na nyingine.

Comments

comments

You may also like ...