Header

Kassim Mganga ushabiki wa mpira wa miguu unavyompiga teke

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania Kassim, Mganga amemetaja aina yake ya ushiriki linapokuja suala la ushabiki wa mpira wa miguu ndani ndani nje ya Tanzania.

Akipiga stori na Dizzim Online, Kassim amesema kuwa nje ya usanii sio shabiki mkubwa wa mpira wa miguu ingawa zipo timu anazozipenda na ikitokea amekutana na mpambano kati ya timu azipendazo anaweza kushiriki kutazama bila mapenzi ya kuwa ni timu ipi ishinde mchezo husika.

“mimi sio shabiki sana wa mpira wa miguu lakini ikitokea zinacheza timu ambazo nazipenda naweza nikaangalia, timu ambazo nazipenda utakuta labda inacheza FC Barcelona, Madrid na hapa Bongo napenda Simba, Yanga na kidogo Azam Fc laki yoyote ikishinda sawa tu, sina noma” Amesema Kassim Mganga.

Hata hivyo, Kassim amesema kikubwa kuhusu ushabiki na mapenzi katika ushabiki wa mpira wa miguu ni kitu kutoka moyoni kitu ambacho kwake haiko sana katika mapenzi yake.

Comments

comments

You may also like ...