Header

Lava Lava azungumzia ‘Bora Tuachane’ na hatua ya watazamaji Million moja Mtandaoni

Msanii wa muziki wa bongo fleva kutoka lebo ya muziki wa WCB Abdul Juma Mangala a.k.a Lava Lava anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Bora Tuachane’ amezungumzia maana kubwa ya video ya wimbo wake kufikisha watazamji Million Moja kwenye mtandao wa Youtube ndani ya kipindi cha mwize moja ikizingatiwa kuwa ni msanii mchanga.

Akizungumza na Dizzim Online Lava Lava amesema kuwa hatua hiyo ni kubwa sana kwa upande wake na lebo kwa ujumla kwakuwa hali ya mapokezi ni kubwana zaidi ni mashabiki kutoka nchi tofauti tofauti wanaendelea kutuma jumbe za kuonesha upendo na kukubali wimbo wake huo wa ‘Bora Tuachane’.

“Mimi nadhani vile wimbo umepokelewa imepelekea wimbo kufikisha viewers million kwa mwezi mmoja, ni suala la kumshukuru Mwenyezi mungu lakini pia kuwashukuru mashabiki wote ambao wamefanya kitu kama hicho kimetokea pia kingine nawaomba waendelee kunisupport kwasababu mimi bila wao siwezi kwenda kokote” Amesema Lava lava.

Hata hivyo Lava Lava ameimbia Dizzim Online kuwa tayari ameshaandaa nyimbo nyingi nzuri na muda wowote ataanza kufuata ratiba ya kuachia nyimbo hata kuongeza kuwa kwa mapokezi anayopata ni wajibu wake kuendelea kufanya kazi nzuri bila kuwaangusha mashabiki.

Comments

comments

You may also like ...