Header

Mayweather na McGregor wahamishia Ulingo kwenye Mitandao ya kijamii(+Video)

Bondia kutoka nchini Marekani Floyd Mayweather pamoja na Conor Mcgregor wameendelea kuonyeshana ubabe nje ya Ulingo kabla ya siku ya Pambano lao baada ya wawili hao kuweka Video fupi katika kurasa zao za mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter na Facebook zikiwaonesha wakiwa wanafanya mazoezi kwa nguvu pamoja na kuwekeana tambo kuelekea pambano lao litakalopigwa Agosti 26 mwaka huu.

Mayweather na McGregor watakutana Ulingoni kwa mara ya kwanza mwezi Agosti.

Mayweather, 40 alianza kwa kuweka video ambayo ameonekana akiwa na kundi la watu wakimshuhudia akijiandaa vyema na kuambatansha maneno yaliyosomeka “Najua sipo kama nilivokuwa miaka 20 iliyopita, sipo kama nilivokuwa miaka 10 iliyopita kiuhalisia sipo kama nilivokuwa miaka 5 iliyopita. Mimi ni Mkongwe wa ngumi ambaye naweka nguvu zangu kwenye kazi nikiwa nimevaa Gloves”. Aliandika Mayweather.

Kwa upande wake Conor McGregor aliweka video fupi katika ukurasa wake wa Twitter akiambatanisha na maneno yaliyosomeka “Hujawai ona hizi muvi” na alimalizia kwa kuweka neno Mzimu.

Mayweather ambae hajawai kupoteza Mchezo wowote kati ya Michezo 49 aliyoshuka ulingoni atakuta na McGregor, 28 katika pambano litakalopigwa katika ukumbi wa  T-Mobile Arena Mjini Las Vegas nchini Marekani Agosti 26 Mwaka 2017.

Comments

comments

You may also like ...