Header

Mazishi ya Prodigy yaudhuriwa na LL Cool J, Remy Ma, Ice-T na Fat Joe kutoka East Coast

LL Cool J, Remy Ma, Ice-T na Fat Joe wamekuwa wachanaji pekee maarufu wa East Coast waliohudhuria kutoa heshima za mwisho kwenye mazishi ya rapa maarufu wa kundi la Mobb Deep ‘Prodigy’ yaliyofanyika mjini New York.

Huduma ya mazishi na ibada ya kumuaga ilifanyika Frank E. Campbell “Funeral Chapel” Upper East Side ambapo washikaji zake wa karibu Questlove na Eddie Huang walikuwepo pia.

Hata hivyo Prodigy alifariki Jumanne ya wiki iliyopita baada ya kugua Ugonjwa wa selimundu (sickle cell disease) tangu kuzaliwa kwake na katika mazishi yake pia rapa mwenzake aambaye walunda kikundi cha Mobb Deep Havoc alihudhuria.

Comments

comments

You may also like ...