Header

Producer au msanii nani huharibu ngoma? Mesen Selekta afafanua

Baada ya mashabiki wa muziki nchini kutaka kujua nani hasa wa kulaumiwa pale ngoma inavyokuwa mbaya; kati ya mtayarishaji wa muziki au msanii mwenyewe, Dizzim Online imezungumza na Mesen Selekta kupata mtazamo wake.

Amesema, “Unajua hapo inategemea, uelewa wangu mimi navyojua muda mwingine inatokana na producer kwasababu producer asipokuwa mzuri hata kama msanii ana uwezo mkubwa bado ataonekana anafanya vibaya kwasababu ya production mbovu.”

“Kule kuna suala la instrumental, mixing kali na mastering nzuri, ingawa muda mwingine producer anaweza kufanya kila kitu vizuri lakini msanii bado akaonekana amebebwa. So ili upate ngoma kali, ni lazima umakini zaidi unahitajika,” ameongeza.

Mesen ameendelea, “Na sometimes producer mwingine anashindwa kumcontrol msanii kumwambia fanya hiki au usifanye hivi au kutokusikiliza idea ya msanii wake. So inakuwa na uwezekano mkubwa sana wa ngoma kuwa mbaya.”

Comments

comments

You may also like ...