Header

Taifa Stars Uso kwa Uso na Bafana Bafana COSAFA

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars itakutana na timu ya Taifa ya Afrika kusini maarufu kama Bafana Bafana Julai 2 mwaka huu katika Mchezo wa Robo fainali wa mashindano ya COSAFA yanayoendelea nchini Afrika kusini baada ya Stars kuweza kufuzu hatua ya makundi.

Taifa Stars ambayo ilitoka sare ya bao moja kwa moja hapo jana dhidi ya Mauritius katika Mchezo wa mwisho wa kundi A, ilimaliza ikiwa kinara wa kundi hilo kwa kukusanya jumla ya alama 5 katika michezo mitatu iliyocheza huku wakiwa sawa na Timu ya taifa ya Angola kwa alama lakini tofauti ya goli moja lilitosha kuwapa tiketi timu ya Taifa ya Tanzania kufuzu.

Group A                     P          W         D         L       GF       GA     Pts
Tanzania
                    3             1           2          0          3          1         5
Angola                         3             1           2          0          1          0         5
Mauritius                   3             0           2          1          1          2         2
Malawi                         3             0           2          1          0          2        2

Mabingwa watetezi ambao ndio wenyeji wa michuano, Timu ya Taifa ya Afrika kusini watacheza mchezo wao wa kwanza na Tanzania katika hatua ya Robo fainali kutokana na taratibu za michuano hiyo huku Zambia, Botswana, Namibia, Lesotho, Swaziland zikianzia pia katika hatua hii ya robo fainali itakayoanza kutimua vumbi Julai 1 mwaka 2017.

Droo ya Robo fainali ilifanyika jana, Botswana dhidi Zambia itakua ndio robo Fainali ya kwanza huku Namibia watacheza dhidi ya Lesotho. Swaziland wanasubiri kinara wa kundi B kati ya timu za Zimbabwe, Msumbiji, Madagasca pamoja na shelisheli, Michezo ambayo itapigwa hii leo.

COSAFA ilitangaza kuondoa kiingilio cha uwanjani kwa hatua yote ya mechi za makundi

Tanzania ni timu mualikwa katika Mashindano hayo, ambayo kocha mkuu wa timu hiyo Salum Mayanga anayatumia kama sehemu ya kuandaa kikosi chake dhidi ya timu ya Taifa ya Rwanda Julai 15 ukiwa ni mchezo muhimu wa kusaka tiketi ya kufuzu kucheza Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani CHAN.

 

Comments

comments

You may also like ...