Header

Ujerumani Yaimaliza Mexico, Fainali kuwavaa Chile kombe la Mabara

Mabingwa wa Dunia, Timu ya Taifa ya Ujerumani imetinga hatua ya Fainali ya Michuano ya Kombe la Mabara baada ya kuibuka na ushindi wa magoli manne kwa moja dhidi ya Mexico hapo jana katika mchezo wa nusu fainali.

Licha ya Kikosi cha Ujerumani kuwakosa nyota wake wengi ambao wameachwa na kocha Joackim Low wakiwemo Manuel Neuer, Jerome Boateng, Mesut Ozil, Toni Kroos pamoja na Thomas Muller bado timu hiyo ilionyesha nguvu dhidi ya Mexico.

Magoli ya Ujerumani yalifungwa na kiungo wa Schalke Leon Goretzka aliyefunga magoli mawili dakika ya 6 pamoja na ya 8 huku Timo Werner kutoka Stuttgart  pamoja na Amin Younes wakiongeza idadi ya magoli mawili huku Fabian akifunga goli pekee la kufutia machozi kwa Mexico.

Ujerumani watakutana na Timu ya Taifa ya Chile katika hatua ya Fainali, Chile walishinda mchezo wao dhidi ya mabingwa wa EURO timu ya Taifa ya Ureno siku ya Jumatano Juni 28 kwa mikwaju ya Penati.

Comments

comments

You may also like ...