Header

Luis Suárez na Neymar kuhudhuria ndoa ya Lionel Messi

Nyota wa klabu ya mpira wa miguu ya Barcelona, Lionel Messi yuko kwenye hatua za mwisho kufunga ndoa na Antonella Roccuzzo mrembo ambaye walikutana na kukua pamoja nchini Argentina.

Ni msaa machache yajayo Messi afanikishe ndoa na mrembo wake huyo ambapo Luis Suárez na Neymar wamepata mualiko rasmi ili kushuruhia pingu za maisha wa wawili hao.

Ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria la ndo ya nyota huyo, wageni wangine waliopata mualiko ni idadi kamili ya watu 260 kwa mujibu wa ripoti ya Gazeti la ‘Clarín’ la Argentina.

Hata hivyo Messi ni mchezaji ambaye alizaliwa kabla ya wakati yaani injiti/kabla ya miezi 9 lakini akiwa ni mwenye umri wa miaka 8 aliwezachukuliwa  na kaanza kulelewa na kukulia katika kituo cha kukuzia vipaji vya mpira wa miguu cha Barca ‘La Masia’.

Comments

comments

You may also like ...