Header

Willy Paul awaonya wapenzi wenye tamaa ya pesa

Msanii wa muziki wa Injili kutoka Kenya na hitmaker wa ngoma ‘Stolia’ na ‘Tamu tamu Remix’ Willy Paul ameachia wimbo unawalenga wale wanaoshindwa kudumu kwenye mahusiano kwasababu ya kuyumba kwa uchumi kwa mtu binafsi.

Baada ya kufanya poa na wimbo ‘Digrii’, kupitia wimbo mpya ‘Pili Pili’ Willy Paul amerekebisha na kuwahasa wote wanaokubali kuwa katika maisha na mtu kama wapenzi pindi anapokuwa na hali nzuri kiuchumi kisha kuvunja mahusiano pindi tu pesa inapoisha na kusema kuwa wazo la wimbo huo ameliweka kwenye sanaa ya muziki kutoka katika tukio lililomtokea moja ya marafiki zake wa karibu, ameiambia  NTV Kenya.

Pili pili ni wimbo uliotayarishwa na Teddy B, mtayarishaji aliyeshiriki kwenye nyimbo nyingi za Willy Paul zilizofanya vizuri ambazo ni Sijafika, Tiga Wana, I Do aliyomshrikisha Alaine kutoka Jamaica na nyingine nyingi.

Comments

comments

You may also like ...