Header

Kanye West ajiondoa kwenye Tidal ya JAY-Z

Kanye West na Tidal ya JAY-Z hawapo pamoja tena. Kwa mujibu wa TMZ, Yeezy amejiondoa kwenye kampuni hiyo kutokana na mgogoro wa kifedha na Tidal imepanga kumshtaki. Vyanzo vimeuambia mtandao huo kuwa Kanye hakuwa na furaha na kampuni hiyo kwa muda mrefu sasa. Kanye amekuwa akilalamika kuhusu kulipwa kiasi cha dola milioni 3 anazoidai Tidal.

Vimesema kuwa mwezi mmoja uliopita, mwanasheria wake alituma barua kwa Tidal akisema kuwa kampuni hiyo imekiuka makubaliano na kuusitisha mkataba. Baada ya wiki mbili, wanasheria wa pande zote mbili walijaribu kukaa chini kuzungumza tofauti hizo lakini juhudi ziligonga mwamba.

TMZ imesema baada ya wiki mbili, mwanasheria wa Kanye West aliwatandika barua nyingine kusisitiza kuwa mkataba huo umeisha. Hata hivyo uamuzi wa Kanye ulitangulia kuachiwa kwa album mpya ya Jay Z, 4:44 ambayo kwenye wimbo mmoja amemchana swahiba wake huyo wa zamani.

Bifu ya Kanye na Tidal ni kutokana na kushindwa kutumizwa kwa ahadi kuwa baada ya album yake, The Life of Pablo kuvutia takriban watumiaji wapya milioni moja kwenye mtandao huo na kwamba alipaswa kulipwa bonus ambayo hadi leo hajapewa. Pia mume huyo wa Kim Kardashian anasema Tidal imegoma kumrudishia gharama zake za kufanya video.

Hata hivyo Tidal imesema Yeezy alishindwa kuwasilisha video zilizohitajika kwenye mkataba huku yeye akidai asingeweza kufanya hivyo bila kupewa bajeti yake. Kampuni hiyo imempiga mkwara Kanye kuwa bado ina mkataba naye na kama akisaini na huduma nyingine ya kusikiliza muziki, watakutana mahakamani.

Yeezy anasema Tidal wakimshtaki, naye anawashtaki vile vile. Hatua hiyo inazidi kutengeneza uadui mkubwa kati ya Kanye na JAY-Z ambao waliwahi kutoa album ya pamoja, Watch The Throne.

Comments

comments

You may also like ...