Header

Ludacris ashtakiwa kwa kosa la kutumia picha

Rapa na Staa wa filamu ya ‘The Fast and the Furious’ Ludacris amejikuta akikalia kiti cha moto yaani amebiliwa na keshi baada ya kutumia picha ya mchoro(Cartoon) iliyoko katika umiliki wa kampuni ya ubunifu wa mawazo katika sanaa ya picha unaolenga hasa wateja wa kike ya ‘LittleThings’ inayosambaza kazi zake kupitia mitandao ya kijamii.

Kesi ya malalamiko kwenda kwa Luda kuhusu picha aliyotumia yalifunguliwa Alhamisi mjini New York ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram alipost picha ya cartoon inayoonyesha mwanamke akijipaka dawa inayonukia ya kuzuia harufu chini ya maziwa yake, picha iliyowahi kupostiwa mtandaoni mwezi Machi ambapo Luda aliabadilisha vitu vichache kama vile rangi na kuweka maneno ya kukuza taarifa kuhusu wimbo wake mpya wa ‘Vitamin D’ taarifa iliyoambatana na link ya kupata wimbo huo kupitia mtandao wa iTune.

Picha aliyotumia Ludacris

Hata hivyo picha hiyo kupitia akaunti ya Instagram ya Luda ilipata likes zaidi ya elfu ishirini kisha akaindoa ambapo kitendo hicho kinatafsiriwa kama wizi na matumizi ya wazo la wabunifu bila ruhusa.

Comments

comments

You may also like ...