Header

Mr. Flavour aifungua kutoka kwenye Album yake Mpya

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria na Staa wa ngoma ‘Obianuju’ Chinedu Okoli a.k.a Mr. Flavour baada ya kuweka sokoni studio album yake ya tano ‘Ijele – The Traveler’ ameachia rasmi ngoma ya kwanza kutoka kwenye album.

Flavour ameanza na wimbo wa kwanza uliotoka sambamba na video yake katika miondoko ya taratibu unaomzungumzia mwanamke na uzuri wake wimbo unaokwenda kwa jina ‘Virtuous Woman’ ambapo video ya wimbo huo imeongozwa na Director Sesan.

Mr. Flavour ujio huu wa album hii ya ‘Ijele’ unafuata baada ya album yake ya 4 yenye ngoma 21 inayokwenda kwa jina ‘Thankful’ iliyotoka mwezi Novemba mwaka 2014.

Comments

comments

You may also like ...