Header

Najuta kuwahi kuwa mrembo wa video za muziki – Masogange

Mrembo wa video za muziki aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini na Afrika kwa ujumla, Agnes Masogange amesema kadri anavyozidi kuwa mkubwa, anajuta kufanya kazi hiyo. Amesema hiyo ndio sababu haonekani kwenye video siku hizi.

Ameiambia Dizzim Online kuwa sababu nyingine ni kuwa boyfriend wake wa sasa hapendi kumuona mrembo wake akiuza sura kwenye video za wasanii wa Bongo. “Sio kwamba wasanii hawanioni hapana wananiona, lakini my boyfriend hapendi kabisa mambo ya kujulikanajulikana, mambo ya video queen
hapendi kabisa,” amesema Aggy.

“Halafu vile vile mi naona wakati nafanya kipindi kile nilikuwa na akili ya kitoto, yaani nilikuwa nataka na mimi niwe star nilijulikane. Nilikuwa nikiona wale dada zetu wanavyoonekana kwenye video na mimi nilikuwa natamani vile. Lakini sasa hivi najuta kwasababu ustaa nao unacost saa zingine,” ameongeza.

“So wajue tu kwamba sasa hivi nimekua mkubwa na mpenzi wangu hapendi.”

Agnes alianza kujipatia umaarufu kwenye video ya Belle 9, Masogange. Kampa Tena ya Reggy ni miongoni mwa video za mwisho mwisho kuonekana.

Comments

comments

You may also like ...