Header

Penny: Instagram kuna mijitu inaboa mpaka basi!

Mtangazaji wa runinga, Penny Mungilwa aka VJ Penny, amesema kuna watu wana shahada za kukura wenzao Instagram. Ameiambia Dizzim Online kuwa mara nyingi amejikuta akiharibiwa siku yake na comments zinazokera kwenye post zake.

“Yaani unakuta mtu anahukumu kitu ambacho hakijui na kipo tofauti na fikra zake. Unakuta mtu ananisema mimi eti napaka make up kila siku, hawajui kama mimi ni mtangazaji wa television so lazim niwe mtu wa kupaka make up kila siku. Sasa baada ya kuuliza anaanza kuongea vitu asivyovijua,” amesema Penny.

“Unakuta nimepost picha nipo na pombe yangu kwasababu mi kiukweli napenda pombe haswaa, mtu anakuja kucomment ‘ooh penny unakunywa wewe una kifua cha Asthma’ sasa watu wote wenye Asthma hawatakiwi kunywa pombe? So watu wanatakiwa kujua mpaka nimeamua kunywa pombe basi nina akili zangu timamu na ninajua madhara yake. Watu wAache kunisema eti kisa Ashtma, nikifanya hivi basi Asthma, nikifanya vile Asthma, ajuwe kwamba sipendi,” ameongeza Penny,

Comments

comments

You may also like ...