Header

Rayvanny amtaja Mwanae Jay Dan kuwa mchango wa mafanikio yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka lebo ya muziki ya WCB na staa wa ngoma ‘Natafuta Kiki’ na ‘Zezeta’, Rayvanny ameuzungumzia uwepo wa mtoto wake wa kwanza wa kiume kuwa mchango mkubwa katika mafanikio ambayo yanaonekana tangu kuzaliwa kwake.

Rayvanny akipiga stori na Dizzim Online Rayvanny ameyasema hayo akisimulia hali ya furaha baada ya mapokezi makubwa jijini Dar es salaam na hatua ya kukutana na mwanae mara baada ya safari yake ya Ushindi ya tuzo ya BET na shughuli zote za muziki nchini Marekani.

Jay Dan

“Yaani Jay Dan ni zaidi ya Tuzo, ni zaidi ya kila kitu, ni zaidi ya kila kitu , ni zaidi ya vitu vingi sana kwenye maisha yangu…nilikuwa nina feelings nzuri sana wakati nimembeba kwasababu toka nimempata ninaona kama kuna vitu vingi ambavyo vinanyooka” Amesema Rayvanny.

Hata hivyo Rayvanny akiwa kwenye safari yake nchini Marekani katika ushiriki na ushindi wa Tuzo ya BET,amefanikisha kurecord nyimbo mbili na Staa wa Marekani Jason Derulo.

Comments

comments

You may also like ...