Header

ZaiiD aitumia jela kurekebisha jamii

Rapa kutoka Sisi Sio Kundi ‘SSK’ ZaiiD a.k.a Mchaff amefafanua matumizi sahihi ya jela na hali ya matabaka yaliyopo kwenye jamii za wanyonge na uwezo katika wazo lake la wimbo mpya wa ‘Umeme Umerudi’.

Akizungumza na Dizzim Online Zaiid ameweka wazi alichokimaanisha na kikubwa kinachoendelea katika jamii na matumizi ya sheria kwa lengo la kuondoa hali ya matabaka ya walio nacho na wasio nacho kwakuwa ni mazingira ambayo amekulia na taarifa zinzaoendelea katika mazingira ya kila siku ya kuishi kwa maana ya kukumbusha na kurekebisha.

“Jela zimejaa wananchi na huku uraiani wamejaa wenye nchi…huu ni mstari ambao nilikuwa influenced na mazingira yangu…unaweza kukuta mtu flani mkubwa au tajiri fulani anakosa fulani kwa ushahidi fulani alafu wao hatujawahi kusikia wameenda jela kwa hiyo lengo langu ilikuwa ni kukumbusha tu kwamba inabidi tufuate sheria” Amesema ZaiiD.

Hata hivyo ZaiiD ametoa sababu na kuzungumzia faida ya kila mmoja kufuata misingi ya sheria na kusema kuwa kama sheria itafuatwa ni njia mojawapo ya kilinda amani ya taifa lolote.

“Kwa hiyo mimi message yangu ni kwamba ki-amani na ki-uhuru inabidi kufuata sheria ili tuwe fair uonevu unapokuwa mkubwa wale wale wananchi wa kawaida rahisi kugeuka waasi na nchi kuingia kwenye machafuko…” Ameongeza.

Comments

comments

You may also like ...