Header

Baba mzazi aingilia mahusiano mapya ya Rihanna

Msanii na staa wa RnB kutoka Marekani Robyn Rihanna Fenty ‘Rihanna’ a.k.a Riri, ameshaonekana katika picha tofauti tofauti kuwa anatoka katika viwanja vya kula bata na tajiri wa kiarabu kwa jina Hassan Jameel anayesemekana kuwa ndiye mpenzi wake ambapo mahusiano hayo yameanza kukutana na vikwazo.

Nje ya kuwa Rihanna kuonekana kuwa na furaha ya kuwa na tajiri huyo, Baba mzazi wa Rihanna ‘Ronald Fenty’ ameonesha kutopendezwa na mahusiano hayo mapya ya mwanae na mwanaume huyo mwenye asili ya kiarabu kwakudai kuwa anapendelea Rihanna awe katika mahusiano na mtu amabaye sio maarufu na awe mwenye asili ya uweusi.

”Rihanna alinambia ana mpenzi siku kadhaa zilizo pita, lakini sikujua ni nani mara nyingi huwa namwambia asiwe na mpenzi msanii au mwana michezo. Aliendelea “Sikujua kama mpenzi wake huyo ni bilionea. Kuwa na pesa nyingi au kuwa na pesa kidogo hakuwezi kukufanya uwe na furaha, unahitaji kitu cha ziada”. Bwana Ronald Fenty aliliambia Sun Magazine.

Kwa mujibu wa maneno ya Ronald Fenty katika kuzungumza na Sun Magazine inaoneana kwa kipindi chote ambacho Rihanna ametoka kimahusiano na watu maarufu katika orodha ya wapenzi wake hakuwa akiyafurahia kwa asilimia kubwa kwakuwa Rihanna amekuwa katika mahusiano na watu wenye umaafuru zaidi.

Comments

comments

You may also like ...