Header

Jeff Horn atamba kumshinda kwa haki Manny Pacquiao

Mwalimu wa zamani wa mchezo wa ngumi aliyempiga Manny Pacquiao ili kushinda taji la uzani wa welterweight ukanda wa WBO amepuuzilia mbali madai kwamba hakufaa kushinda taji hilo katika pigano la tarehe 2 Julai.

Jeff Horn akichukua alama kwa Manny Pacquiao

Baada ya mwalimu huyo Jeff Horn na bingwa huyo wa dunia mara nane kumshinda Manny Pacquiao, kufuatia wingi wa pointi katika mji wa Brisbane, Australia, Mkufunzi wa Manny Pacquiao na watu maarufu akiwemo Lennox Lewis na Kobe Bryant wamekosoa matokeo hayo.

“Kutakuwa na maneno kwamba nilikuwa na bahati ama chochote kile, kutakuwa na wale watakaosema kwamba sikufaai kushinda, lakini ninahisi kwamba nilishinda pigano hilo kihalali” Jeff Horn Aliwaambia maripota siku ya Jumatatu.

Hata hivyo kocha wa Pacquiao nchini Australia Justine Fortune aliulalamikia uamuzi wa refa na majaji kuwa haukuwa wa haki katika pigano hilo

Comments

comments

You may also like ...