Header

Nahreel ataja kinachoikwamisha shule yake ya muziki

Nahreel amesema kutingwa na kazi nyingi kunaikwamisha shule yake ya muziki kuendelea kama alivyokuwa amepanga. Nahreel ambaye yeye na Aika wanaunda kundi la Navy Kenzo walitumbuiza mwishoni mwa wiki mjini Goma, DRC.

“Shule yangu ilikuwa na wanafunzi wengi tu, lakini kadri siku zinavyoenda kazi zinakuwa nyingi. Na kama ambavyo mnajua mimi nafanya kazi nyingi, kuna production na muda huo huo ni msanii pia, kwahiyo ule muda wa kuwepo pale kuangalia na kuwafanya wanafunzi wakue mpaka unavyotaka wewe inakuwa ni ngumu kidogo. Lakini huo mpango utaendelea, ni kuweka tu mambo sawa sitoacha kusaidia wengine kutimiza ndoto zao kama mimi.”

Mwaka huu Navy Kenzo wamefanikiwa kurudi tena kwenye kipindi cha Coke Studio Afrika.

Comments

comments

You may also like ...