Header

RockStar4000 yamtangaza AliKiba kuwa Mkurugenzi

Msanii wa muziki wa Bongo fleva, na staa wa pili Afrika kusainiwa ROCKSTAR4000 Ali Saleh Kiba a.ka jana usiku ametangazwa rasmi kuwa mkurugenzi na sehemu ya wamiliki wa kampuni ya Rockstar4000 Music Entertainment and Rockstar Television.

Kampuni hiyo inayojishughulisha na utengenezaji wa vipindi vya mastaa tofauti kutoka nchi mbalimbali na kuvisambaza katika vituo vya Televisheni za kimataifa imechukua mkondo wa kumtangaza Ali Kiba baada ya msanii huyo kufanya kazi na kampuni hiyo kwa takribani miaka 6.

Hakika ni hatua kubwa wa Ali Kiba na heshima kwa taifa la Tanzania kwakuwa sasa anakuwa sehemu ya wasanii waliochini ya Rockstar4000 na kupewa nafasi kama Mkurugenzi wa Vipaji na Muziki wa kampuni hiyo.

Dalili za kuja kitu kikubwa na cha kishinda zilianza jana jana jioni kupitia mtandao wa Instagram ambapo Alikiba aliwatangazia mashabiki wakae mkao wa kula kwani yupo mbioni kuwapa taarifa mhimu. Kupitia instagram aliandika hivi

”My Superfans! I will be making an exclusive announcement today with #RockstarTV – Register and Log on to https://www.younow.com/RockstarTV for the news and I will talk to all my fans LIVE by video stream! – Stand By for the Time will be announced soon…! Link on BIO wait for it.

Na walipoenda mubashara kupitia mtandao wa Instagram taarifa rasmi iliyotoka ni hiyo ya Ali Kiba kuwa mkurugenzi wa RockStaa4000 ambapo alisikika akisema ‘Ni partner sasa hivi, mimi Jay na Seven Thank You so much for Support”.

Comments

comments

You may also like ...