Header

Youngkiller ashindilia zaidi kuhusu kumdiss Nay wa Mitego

Rapa Youngkiller Msodoki anayefanya vizuri na ngoma ‘Sinaga Swagga Remix,’ ametoa maelezo ya ni haina gani ya msanii anayeweza kujibu kwa diss na sababu zipi zinaweza kumsukuma kujibu kwa lolote linalomhusu katika maisha ya muziki wake.

Akipiga stori na Dizzim Online Killer amesema kuwa sio kila atakapodiss-iwa atachukua jukumu la kujibu tofauti na msanii atakaye mdiss kwa nia ya kupotosha jamii na kutoa maoni tofauti na ukweli kwa hali husika huku akimtolea mfano Nay wa Mitego kwa mtaja kuwa alistahili kujibiwa kwa madai yake binafsi kuwa alipotosha.

“kiukweli kabisa siwezi kumdiss kila atayenidiss, unaangalia kwanza na mtu kakudiss kwa namna gani. Kama mtu kakudiss kwa facts anaagalia sehemu ambayo umekosea unarekebisha unaendelea na harakati zako. Lakini kama mtu kakudiss katika kuipotosha jamii lakini kama mtu kakudiss katika upumbavu, katika kuipotosha jamii huyo lazima umjibu kwasababu atakauwa ni mpumbavu” Amesema Youngkiller.

Hata hivyo Youngkiller ameongeza kuwa kwa kipande kilichosikika akitajwa na Nay wa Mitego katika wimbo wa ‘Moto’ ni kama kukosewa heshima hivyo hakuona sababu za kukaa kimya nan do maana amechukua maamuzi ya kumjibu kwa wimbo wake wa ‘True Boya’.

 

Comments

comments

You may also like ...