Header

Future kuongozana na Wizkid kwenye Tour yake

Msanii na mkali wa ngoma iliyochukua tuzo ya Billboard 2017 kupitia kipengele cha Top R&B Song ‘Come Closer’ ngoma iliyoshinda aliyomshirikisha Staa mkanada Drake ‘Wizkid’ amekula shavu lingine kuwa la kutumbuiza katika ziara ya rapa Future ‘The Future Hndrxx Tour’.

Ziara itakayoanza tarehe 8, Julai mwaka huu na moja ya Staa kutoka Afrika aliyepata heshima ya kushiriki ni Wizkid ambapo hilo limethibitika kupitia ukurasa wake wa Twitter mara baada ya kupost na kuonesha furaha yake ya kuwa katika orodha ya watakao toa burudani katika ziara hiyo ya Future.

Hii ni post ya Future iliyotoa taarifa rasmi ya kuanza na kumalizika kwa Ziara hiyo.

Hii ni post ya Wizkid iliyothibitisha uwepo wake katika ya ‘The Future Hndrxx Tour’

Wizkid ni msanii mkubwa Afrika ambaye amepata fursa kubwa za kupeleka muziki wake kimataifa zaidi ikiwa ni pamoja na kolabo kubwa na mastaa wakubwa Duniani. Wizkid ameshafanikisha kazi na mastaa kama French Montana, Chris Brown, Drake, Trey Songz, Diplo, Ty Dolla Sign, Legendury Beatz na wakali wengine.

Comments

comments

You may also like ...