Header

Miami Heat yamuondoa Bosh na kustaafisha Jezi yake

Timu ya kikapu ya Miami Heat imethibitisha kumuondoa kikosini Mchezaji wao Chris Bosh aliyetumikia timu hiyo kwa zaidi ya miaka mitano kutokana na kugundulika na tatizo la ugonjwa wa kuganda damu mwilini (Blood Clot) huku ikidaiwa pia kuistaafisha Jezi yake namba 1.

Bosh, 33 alijiunga na Miami mwaka 2014 akitokea Toronto Raptors, punde tu baada ya LeBron James kurejea Cleveland Cavaries. Ameitumikia Miami kwa kipindi cha miaka 6 na kuisaidia timu hiyo ya kikapu kutwaa Ubingwa wa NBA mara mbili mfululizo yaani mwaka 2012 na 2013 akitokea katika timu ya Toronto Raptors.

Mchezaji huyo wa kikapu amekosa msimu mzima uliopita 2016/2017 kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa huo aliogundulika nao mwaka 2015. Amecheza misimu 13 NBA, Saba akiwa na Raptors 6 akiwa na Miami.

Licha ya kuachwa na Miami Heat timu hiyo imetangaza kuendelea kumlipa Chriss Bosh Mshahara wake ambao ni zaidi ya dola za Kimarekani 52.1 kwa kipindi cha Mkataba wake uliobaki wa Miaka miwili.

Comments

comments

You may also like ...