Header

Ronaldo; Mwanamichezo anayeongoza kuingiza Pesa nyingi Instagram

Mshindi mara nne wa Tuzo ya Ballon D’or Cristiano Ronaldo ndiye Mwanamichezo anayeongoza kuingia pesa nyingi zaidi kupitia Mtandao wa kijamii wa Instagram, Takwimu hizi ni kwa Mujibu wa Kampuni inayoshughulika na Masuala ya Mtandao husussani Mitandao ya kijamii ya Hopper ya nchini Uingereza .

Getting a bit to much exposure 😃

A post shared by Cristiano Ronaldo (@cristiano) on

Ronaldo ambaye ni Mwanamichezo mwenye wafuasi wengi zaidi Duniani katika mitandao ya kijamii akiwa na Jumla ya Wafuasi Millioni 104 ameripotiwa kuingiza kiasi cha pesa ambacho ni zaidi ya Paundi 308,000 kwa Post moja anayoweka kwenye Mtandao wa Instagram.

Pia nyota huyo kutoka nchini Ureno ni nyota wa tatu katika orodha ya watu maarufu wenye Wafuasi wengi zaidi nyuma ya Mwanadada Selena Gomez mwenye wafuasi Milioni 122 ambaye anaingiza kiasi cha Dola za kimarekani 550,000 pamoja na Kim Kardashian mwenye wafuasi Milioni 100 akiingiza kiasi cha dola za kimarekani 500,000.

Katika Orodha hiyo iliyotolewa na Kampuni ya Hopper ni Wachezaji wawili tu ambao wapo katika Orodha hiyo ambao ni Cristiano Ronaldo ambaye anashika nafasi ya tatu pamoja na Nyota wa mpira wa kikapu kutoka Cleveland Cavaries LeBron James ambaye anashika nafasi ya kumi akiwa na Jumla ya Wafuasi Milioni 30.7 akiingiza kiasi cha Dola za Kimarekani 120,000.

Comments

comments

You may also like ...