Header

Exclusive: Timbulo akata mzizi wa fitina wa kwanini anafululiza nyimbo

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Staa wa ngoma ya ‘Mfuasi’ Timbulo, ametoa jibu la swali ambalo baadhi walijiuliza kuwa ni kwanini anafululiza nyimbo ndani ya muda mfupi kufuatia ujio wa ngoma yake nyingine mpya inayokwenda kwa jina la ‘Mshumaa’ ngoma iliyofuata baada ya ‘Ndotoni’ iliyotoka mwezi jana.

Swali hilo, Timbulo amelijibu alipokuwa akipiga stori na Dizzim Online ambapo amesema kuwa tayari anazo nyimbo nyingi mkononi na ni nzuri sana, kitu pakee cha kufanya kuhusu ngoma hizo ni kuwapa mashabiki na kingine ni kwa muda alipumzika hivyo kishindo cha kurudi kwake kitaenda sambamba na ngoma baada ya ngoma.

“Kilichonifanya nifanye back to back ni kwasababu nimegundua kwamba demand ya watu ni kubwa zaidi kuliko kazi ambazo mimi nimezitoa kwahiyo nikaona kwamba si vibaya. Watu wanapenda kazi zangu kwanini niwanyime utamu sasa, wacha niwape kile mbacho wanastahili kwasababu mimi nafanya kwa ajili yao na ndo maana naona bora nifanye kwasababu wanahitaji” Amesema Timbulo.

Hata hivyo Timbulo amebainisha kuwa katika kufanya utafiti wa kimuziki amegundua moja ya njia za msanii kuwa mkubwa katika sanaa yake anahitaji kufanya kazi nyingi nzuri ili pate nafasi ya kupewa sikio na kitu ambacho anakifanyia kazi kwa sasa.

“Kitu kikubwa zaidi nahitaji kuwa na ukubwa, nahitaji kuwa mkubwa. Siwezi kupata ukubwa kama sitakuwa na kazi nyingi” Aliongeza.

Comments

comments

You may also like ...