Header

Gabriel Jesus kuikosa Man Utd

Mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus anatarajia kukosa baadhi ya Michezo ya maandalizi ya msimu ujao ukiwemo ule wa ‘Derby’ dhidi ya Manchester United kutokana na kusumbuliwa na jeraha katika eneo la jicho alilopata wakati anatumikia timu yake ya Taifa ya Brazil.

Manchester City itaweka kambi nchini Marekani kushiriki Mahindano ya ICC Championship yatakayoshirikisha timu mbalimbali kutoka Barani Ulaya na itacheza na Manchester United Julai 20 katika Uwanja wa NRG uliopo Huston nchini Marekani Mchezo ambao Jesus ataukosa.

Jesus, 20 aliumia katika Mchezo wa Kirafiki dhidi ya Argentina mwezi Juni mwaka huu baada ya kugongana na Mchezaji mwenzie wa Manchester City anayechezea timu ya Taifa ya Argentina beki Nicolas Otamendi na kuumia eneo la jicho, alitolewa uwanjani kwa kutumia Machela.

Kwa Mujibu wa Daktari kutoka nchini Brazil ambaye anamuuguza Jesus, Dr Pagura staa huyo atakuwa nje kwa wiki tatu kabla ya kujiunga na Manchester City.

“Sio tatizo kubwa sana, hatafanyiwa upasuaji kwa tatizo hili. anahitaji kuwa chini ya uchunguzi kwa muda wa takribani wiki tatu”. Alisema Dakatari huyo alipohojiwa na kituo cha Televisheni cha Esp_Interativ cha nchini Brazil

Gabreil Jesus alijiunga na Manchester City Mwezi Januari akitokea katika klabu ya Palmeiras ya nchini Brazil. Tangu ajiunge na City amekua akisumbuliwa na majeraha, ambayo yamemsababishia kukosa baadhi ya Michezo msimu uliopita kati ya mwezi wa pili mpaka wa tatu. Alivunjika mfupa wa Mguu wa kushoto mapema mwezi Machi mwaka huu.

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...