Header

Lacazette ataja kilichomvutia kujiunga Arsenal

Mshambuliaji mpya wa Klabu ya soka ya Arsenal Alexandre Lacazette ametaja sababu kubwa iliyomfanya ajiunge na Klabu hiyo katika kipindi hiki cha Dirisha kubwa la usajili, kuwa ni Mafanikio na historia nzuri waliyowai kupata wachezaji kutoka Ufaransa waliotumikia Arsenal.

Lacazette, 26 ambaye amejiunga na Arsenal akitokea klabu ya Lyon kwa ada ya Paundi Milioni 46.5 na kuwa Mchezaji Ghali katika klabu ya Arsenal ametaja sababu hiyo alipohojiwa kwa mara ya kwanza baada ya kutia saini Mkataba wa miaka mitano kuitumikia Klabu hiyo.

“Kiukweli nina Furaha sana kujiunga na Arsenal, Arsenal ni Klabu kubwa na ni kongwe sana. Sababu ya kujiunga na Arsenal ni kutokana na Mafanikio ambayo wachezaji wa Ufaransa wamekua wakipata hapa, kama vile Thierry Henry pamoja na wachezaji wengine kutoka Ufaransa lakini pia kocha yupo katika klabu hii kwa muda mrefu na kuna wachezaji baadhi kutoka Ufaransa ambao bado wanafanya vizuri pia na nipo tayari kuisaidia Arsenal ili ishinde mataji mengine”. Alisema Lacazette.

Nyota kadhaa kutoka Ufarana wamewai kuitumukia Arsenal kwa Mafanikio makubwa wakiwemo Patric Viera William Gallas, Robert Pires pamoja na Thierry Henry ambao miongoni mwao walikuwepo katika kikosi cha Arsenal kilichotwaa ubingwa bila kufungwa msimu wa 2003-2004.

Mshambuliaji huyo ni Mchezaji wa pili kusajiliwa na Arsenal mwaka huu baada ya Sead Kolasinac kusajiliwa akitokea klabu ya Schaike 04 ambao wote wanatarajia kusafiri na kikosi kizima kuelekea nchini Australia kujiandaa na msimu ujao 2017/2018.

 

 

Comments

comments

You may also like ...