Header

Nay wa Mitego kumrudisha Godzillah kwa lengo la kumuepusha na Ngada, Bifu nje nje?

Rapa na mmiliki wa lebo ya muziki ya Free Nation aliyerudi kwenye headlines za diss na ngoma yake ya ‘Moto’ Nay wa Mitego, ameingilia bifu ya kimuziki na kutetea kauli yake ya kuwa Bill Nas anampa Stress rapa Godzilla katika muendelezo wa bifu la kimuziki kati ya Zillah na rapa Wakazi.

Kupitia ukurasa wa Instagram Nay ameutetea wimbo wake wa ‘Moto’ kuwa kila aliyechanwa amechana kwa kuzingatia ukweli kupitia wimbo wake huo wapo walipanic, katika kuwaomba mashabiki wataje wanayejua kuwa alimchana na akapanic aliwafungulia orodha kwa kuanza na Godzillah ambapo amesisitiza kuwa ni kweli Godzillah amepotea kwenye game la muziki na kumkaribisha katika studio zake za Free Nation kwa kumuahidi kuwa akifanya kazi naye katika studio yake itamrudisha kwenye game.

Godzillah baada ya kukutana na maneno hayo ya Nay wa Mitego, alitumia ukurasa wake wa Twitter kufichua siri ya sababu za kwanini Nay anamchimba, Godzillah hakusita aliamua kufichua na kubainisha kuwa Nay alishamtaka wafanye ngoma ya mabishano ombi ambalo Zillah kwa mujibu wa Tweet yake alilikataa kwa kutoa sababu kuwa ni wazo ambalo Nay ameshafanya kalba kabla.

Vile vile Zillah hakuishia hapo alionesha kuwa anabadilisha ulelekeo wa kujibu kuhusu jambo lenye sura ya bifu na kushauri kuwa ni muda wa muziki mzuri kufanyika.

Comments

comments

You may also like ...